This is featured post 1 title
Replace these every slider sentences with your featured post descriptions.Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha - Premiumbloggertemplates.com.
jiji la mwanza
Replace these every slider sentences with your featured post descriptions.Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha - Premiumbloggertemplates.com.

This is featured post 3 title
Replace these every slider sentences with your featured post descriptions.Go to Blogger edit html and find these sentences.Now replace these with your own descriptions.This theme is Bloggerized by Lasantha - Premiumbloggertemplates.com.

Sunday, 23 August 2015


Kama kawaida uzinduzi wa kampeni za CCM kuelekea uchaguzi mkuu wa Urais, Ubunge na madiwani, uzinduzi wa CCM ambao ulipambwa na uwepo pia wa makada wa CCM
kutoka katika tasnia ya filamu na wasanii wa bongofleva pia walikuwepo
licha ya kutokana na ufinyu wa muda waliopata nafasi ya kuperform hadi
sasa ni Peter Msechu, Yamoto Band na Diamond Platnumz sambamba na timu ya watu wake.
Kwa upande wa wasanii wa filamu na
baadhi ya wasanii wa muziki wa bongofleva wao walipanda katika stage na
kuimba wimbo wa taifa kwa pamoja.
Hizi ni picha zingine kutoka Jangawani


Klabu ya FC Barcelona imeshuka uwanjani kucheza mechi yake ya kwanza Ligi Kuu Hispania, FC Barcelona imeingia uwanjani kucheza na klabu ya Athletic Bilbao ikiwa ni wiki moja imepita toka ipokee kipigo kutoka kwa Athletic Bilbao katika mchezo wa Super Cup.

August 23 FC Barcelona imerudi kucheza mechi ya Ligi Kuu na Athletic Bilbao ila imefuta uteja wa kukosa ubingwa wa Super Cup ila katika mchezo wa Ligi Athletic Bilbao imekubali kipigo cha goli 1-0, goli pekee la dakika ya 54 kutoka kwa Luis Suarez liliwafanya FC Barcelona kuondoka na point 3 muhimu.






Tuesday, 18 August 2015


SIKU mbili baada ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), kumvua Ukamanda Mkuu, mwanasiasa mkongwe nchini, Mzee Kingunge Ngombale Mwiru, uamuzi huo umepokewa tofauti na mgombea urais kwa tiketi ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Bw. Edward Lowassa.
Tamko
la UVCCM ambalo lilitolewa na Katibu Mkuu wa umoja huo,Sixtus Mapunda,
lilisema wamefikia uamuzi huo kutokana na tabia, mwenendo wa Mzee
Kingunge aliounesha hivi karibuni tofauti na maadili pamoja na taratibu
za CCM.
Umoja huo ulipendekeza vikao vya CCM, kuuangangalia upya uanachama wake na kuchukua hatua kubwa zaidi.
Bw.
Lowassa ambaye pia ni mgombea urais anayeviwakilisha vyama vinavyounda
Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA), alisema CCM itapata laana kama
itaridhia kuondolewa kwa Mzee Kingunge.
Akiwahutubia
mamia ya wafuasi wa UKAWA katika Viwanja vya Kibandamaiti, Mjini
Zanzibar, jana ambako alikwenda kutambulishwa na kutafuta wadhamini, Bw.
Lowassa alisema Mzee Kingunge ni mmoja kati ya wazee muhimu ndani ya
CCM.
"Nasikitika sana kwa hatua kali alizochukuliwa Mzee Kingunge, kama isingekuwa yeye, CCM isingefika hapo ilipo, watapata laana," alisema.
Mapokezi yake
Lowassa
aliwasili Zanzibar jana asubuhi akitokea jijini Mwanza kwandege ya
kukodi akiwa na viongozi wengine wa UKAWA pamoja na mgombea mwenza, Bw.
Juma Duni Haji.
Baada
ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Zanzibar, msafara huo
ulipokewa na Katibu Mkuu wa CUF Taifa ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa
Rais Zanzibar, Maalim Seif Sharif Hamad.
Akihutubia
mkutano huo, Lowassa aliwaambia Wazanzibar kuwa atahakikisha
anazingatia taratibu za kisheria ili Masheikh wa Jumuiya ya Mihadhara ya
Kiislamu (Uamsho) wanaoshikiliwa katika mahabusu jijini Dar es Salaam,
wanapata haki zao.
Ahadi hiyo ya Lowassa ilisababisha umati huo kulipuka kwa furaha na vifijo huku ukimuita `Rais, Rais, Rais.
Alisema kwa mara zote alizokwenda Zanzibar, hajawahi kushuhudia umati mkubwa kama aliouona jana.
Lowassa
alisema amekwenda Zanzibar kuomba dhamana ya wananchi na kurudia kauli
yake kwamba anawania urais kwa kuwa anauchukia umaskini.
“Nataka
kuwahakikishia Watanzania popote kwamba mabadiliko yataletwa na vyama
vya upinzani. Nimetembea sehemu mbalimbali nimeona wananchi wanataka
mabadadiliko ya uongozi,” alisema.
Kuhusu
Katiba, alisema yeye ni muumini wa Serikali Tatu zitakazosaidia
kuimarisha Muungano na kwamba msimamo wake huo aliouonyesha tangu miaka
ya 90 wakati wa harakati za kundi la G55.
Alisema suala hilo litafafanuliwa vizuri wakati wa uzinduzi wa ilani ya uchaguzi Jumamosi wiki hii na wakati wa kampeni.
Hata hivyo, Lowassa alisema njia ya kuiondoa CCM madarakani, ni kwa kupiga kura na wananchi wajiandae pia kulinda kura.
Masheikh waliofungwa
Alisema
Masheikh mkoani Mwanza walimwomba azungumzie jambo hilo na kwamba
atakachofanya atakapoingia madarakani, atazingatia taratibu za kisheria
kufuatilia stahili zao.
Mpekuzi blog


MFANYABIASHARA wa duka la vipuri vya magari mjini Tarime mkoani Mara, Tumaini Jacob amefikishwa katika Mahakama ya Wilaya akituhumiwa mauaji ya askari wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).
Anadaiwa
kumuua askari huyo wa Kikosi cha Nyandoto, Roja Elias kwa kumpiga
risasi tumboni wakati wakiwa baa moja mjini hapa baada ya kutokea ugomvi
wa kunyang’anyana mwanamke ambaye ni mhudumu wa baa hiyo. Alisomewa
mashitaka hayo jana mbele ya Hakimu Mkazi wa Mahakama ya Wilaya Tarime,
Marther Mpaze.
Mwendesha
Mashitaka wa Polisi, George Lutonja alidai kuwa Jacob (45) Agosti 17
usiku saa 6 .30 wakati akiwa baa na Hoteli ya NK, kulitokea ugomvi kati
yake na askari huyo.
Alidai
katika ugomvi huo, Tumaini alichomoa bastola yake na kumpiga risasi
Roja tumboni na kutokea mgongoni. Majeruhi huyo alikimbizwa Hospitali ya
Wilaya ambapo hali yake ilizidi kuwa mbaya na kuhamishiwa Hospitali ya
Rufaa Bugando ambapo mauti yalimkuta akipatiwa matibabu katika hospitali
hiyo ya Bugando Mwanza.
Mtuhumiwa huyo Tumaini hakutakiwa kujibu lolote, kwani mahakama hiyo haina uwezo wa kusikiliza kesi za mauaji.
Mpekuzi blog
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )


CHAMA
cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kimetoa orodha ya majina 138 ya
wanachama walioteuliwa na Kamati Kuu ya chama hicho kugombea ubunge wa
majimbo ya uchaguzi.
Orodha
ya majina hayo ya wanachama walioteuliwa kugombea ubunge katika majimbo
hayo, imesainiwa na Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika kwa niaba
ya Katibu Mkuu.
Taarifa
imeeleza kuwa majimbo ambayo hayatakuwa kwenye orodha hiyo yatatolewa
baada ya kukamilika kwa mashauriano ndani ya Umoja wa Katiba ya Wananchi
(UKAWA).
Katika
mgawanyo wa UKAWA wa majimbo 253 Kati ya 265 ya kuwania ubunge, Chadema
imeongoza kwa kupata majimbo 138 (54%), ikifuatiwa na CUF majimbo 99
(29% yakiwemo 49 ya Zanzibar), NCCR-Mageuzi majimbo 14 (5.5%) na NLD
majimbo matatu (1.2%).
Ifuatayo ni orodha kamili ya majina ya wanachama wa Chadema walioteuliwa kugombea ubunge katika majimbo hayo.
Mara
- Rorya STEVEN J OWAWA
- Tarime Mjini ESTHER N MATIKO
- Tarime Vijijini JOHN HECHE
- Musoma Vijijini ZAKARIA MBULA CHIRAGWILE
- Butiama YUSUPH R KAZI
- Bunda Mjini ESTHER BULAYA
- Mwibara HARUN D CHIRIKO
- Musoma Mjini VINCENT J NYERERE
- Bunda Vijijini SULEIMAN DAUDI
Simiyu
- Bariadi GODWIN SIMBA
- Maswa Magharibi ABDALA PATEL
- Maswa Mashariki SYLVESTER KASULUMBAYI
- Kisesa MASANJA MANANI
- Meatu MESHACK OPULUKWA
- Itilima MARTINE MAGILE
Shinyanga
- Msalala PAULO MALAIKA
- Kahama Mjini JAMES LEMBELI
- Kahama Vijijini (Ushetu) SIMON BUKAKIYE ISAYA
- Shinyanga Mjini PATROAS PASCHAL K
- Kishapu FRED T MPENDAZOE
Mwanza
- Ukerewe JOSEPH MKUNDI
- Magu KALWINZI NGONGOSEKE
- Nyamagana EZEKIA D. WENJE
- Buchosa MARTINE KASWAHILI
- Sengerema HAMIS TABASAMU
- Ilemela HIGHNESS KIWIA
- Misungwi LEONIDAS KONDELA
Geita
- Bukombe PROF. KULIKOYELA KAHIGI
- Busanda ALPHONCE C MAWAZO
- Nyang’wale GEORGE MABULA
- Chato DR. BENEDICT LUKANIMA
- Mbogwe NICODEMUS H MAGANGA
Kagera
- Karagwe PRINCE RWAZO
- Kyerwa BENEDICT MTUNGIREHI
- Bukoba Mjini WILFRED LWAKATARE
- Muleba Kaskazini ANSBERT NGURUMO
- Muleba Kusini ALISTIDES KASHASILA
- Biharamulo DR. ANTHONY MBASSA
Mbeya
- Lupa NJELU KASAKA
- Songwe MPOKI MWANKUSYE
- Mbeya Mjini JOSEPH MBILINYI
- Kyela ABRAHAM H MWANYAMAKI
- Rungwe JOHN D MWAMBIGIJA
- Busokelo BONIPHACE A MWAMUKUSI
- Mbozi PASCHAL HAONGA
- Momba DAVID E SILINDE
- Mbeya Vijijini ADAM NZELA
- Tunduma FRANK MWAKAJOKA
- Vwawa FANUEL MKISI
Iringa
- Ismani PATRICK OLE SOSOPI
- Kalenga MUSSA L MDEDE
- Mufindi Kaskazini JUMANNE K MASONDA
- Iringa Mjini PETER MSIGWA
- Kilolo BRIAN KIKOTI
- Mafinga Mjini WILLE MUNGAI
Njombe
- Njombe Kusini EMMANUEL MASONGA
- Lupembe (Njombe Kask) EDWIN E SWALE
- Wanging’ombe DISMAS A LUHWAGO
- Makete JACKSON T MOGELA
- Ludewa ATHROMEO MKINGA
- Makambako ORAPH MHEMA
Rukwa
- Nkasi Kusini ALFRED DANIEL SOTOKA
- Kwela DANIEL NAFTAL NGOGO
- Nkasi Kaskazini KESSY SOUD
- Sumbawanga Mjini SADRICK MALILA
- Kalambo VICTOR MATENI
Tanga
- Kilindi JERADI K MREMA
- Muheza ERNEST MSINGWA
- Korogwe AMANI H KIMEA
- Korogwe Vijijini EMMANUEL KIMEA
Kilimanjaro
- Rombo JOSEPH SELASIN
- Same Magharibi CHRISTOPHER S MBAJO
- Same Mashariki NAGENJWA KABOYOKA
- Moshi Mjini JAFARY P MICHAEL
- Hai FREEMAN A MBOWE
- Siha DR. GODWIN MOLLEL
Arusha
- Arumeru Mashariki JOSHUA NASSARI
- Arumeru Magharibi GIBSON MESIYEKI
- Arusha Mjini GODBLESS LEMA
- Longido ONESMO OLE NANGOLE
- Monduli JULIUS KALANGA
- Karatu WILLE QAMBALO
- Ngorongoro ELIAS NGORISA
Manyara
- Simanjiro JAMES KINYASI OLE MILLYA
- Mbulu Vijijini MIKEL PETRO AWEDA
- Hanang MAGOMA RASHID DERICK
- Babati Mjini PAULINE P GEKUL
- Babati Vijijini LAURENT SURUMBU TARRA
- Kiteto KIDAWA ATHUMANI IYAVU
- Mbulu Mjini PAULO HERMAN SULLE
Dar es Salaam
- Ubungo SAED KUBENEA
- Kawe HALIMA JAMES MDEE
- Ukonga MWITA MWIKWABE WAITARA
- Ilala MUSLIM HASSANALI HEIDERALI
- Kibamba JOHN JOHN MNYIKA
Pwani
- Chalinze MATHAYO TM. TORONGEY
- Kibaha Mjini MICHAEL PAUL MTALY
- Kibaha Vijijini EDITHA BABBEIYA
Morogoro
- Mikumi JOSEPH HAULE
- Morogoro Kusini DAVID LUKAGINGIRA
- Kilombero PETER E LIJUALIKALI
- Mlimba SUZAN L. KIWANGA
- Mvomero OSWALD MLAY
- Ulanga Magharibi ALPHONCE MBASSA
- Ulanga Mashariki PANCRAS KONGOLI
- Morogoro Mjini MARCOSSY ALBANIE
Dodoma
- Kongwa ESAU NGOMBEI
- Dodoma Mjini SINGO BENSON KIGAILA
- Bahi MATHIAS LYAMUNDA
- Chilonwa JOHN CHOGONGO
Singida
- Iramba Magharibi JESCA KISHOA
- Iramba Mash(Mkalama) OSCAR KAPALALE
- Singida kaskazini DAVID DJUMBE
- Singida Mashariki TUNDU A LISSU
- Singida Magharibi MARCO ALLUTE
- Manyoni Magharibi LUPAA DONALD
- Manyoni Mashariki ALLUTE EMMANUEL
Tabora
- Nzega Mjini CHARLES MABULA
- Igunga NG’WIGULU KUBE
- Urambo SAMWELI NTAKAMLENGA
- Ulyankulu DEUS KITAPANDYA NGERERE
- Sikonge SAID NKUMBA
- Manonga ALLY KHALFANI NGUZO
Katavi
- Mpanda Mjini JONAS KALINDE
- Mpanda Vijijini MUSSA MASANJA
- Katavi GEORGE SAMBWE
- Nsimbo GERALD KITABU
- Kavuu LAURENT SENGA MANGWESHI
Kigoma
- Kigoma Kaskazini DR. YARED FUBUSA
- Kigoma Mjini DANIEL LUMENYELA
Ruvuma
- Peramiho ELASMO MWINGIRA
- Mbinga Magharibi/Nyasa CUTHBERT S. NGWATA
- Mbinga/Mbinga Vijijini EDWIN B AKITANDA
- Songea Mjini JOSEPH FUIME
- Madaba EDSON MBOGORO
Mpekuzi blog
Tupe Maoni Yako( Matusi Hapana )

Subscribe to:
Posts (Atom)